KIM KARDASHIAN ASIFIA UGONJWA WA MAFUA

Posted on : April 20, 2017.   22 Views. 
Mwanamitindo Kim Kardashian amesema amepungua uzito baada ya kuugua mafua.Kim ambaye ni mke wa Rapa Kanye  West,west alisema licha ya kuumwa mafua amefurahia ugojwa huo umemsaidia kupungua uzito jambo ambalo ilikuwa akihitaji kwa muda mrefu. Nyota huyo ambaye ni mama wa watoto wawili alisema kupungua kwa uzito kutamwezesha kufanya vizuri kwenye onesho la mavazi la Met Gala litakalofanyika Mei Mosi mwaka huu. ''Tangu nipungue uzito nafanya kazi bila kuchoka nimekuwa mwepesi na hata nikivaa nguo zinanikaa vyema''alisema Kim Alisema kwa sasa ameandaa ratiba maalumu ya vyakula atakavyo kuwa  akila na ataendelea kupunguza uzito hadi hapo atakapoona umbo lake limekaa vizuri.
       

 
Social Media

© 2016 PRO24 DJS | All Rights Reserved!