0%

LAVA LAVA AELEZA ANAVYOMKUBALI YOUNG KILLER

Posted By: author_4 On:


Msanii mpya ndani ya Lebo ya WCB, Lava Lava amesema alikuwa anamfahamu na kumfuatilia Young Killer toka muda mrefu wakati akiwa THT huku akidai kuna vitu alishafanya pamoja na rapa huyo.

Muimbaji huyo anayefanya vizuri na wimbo ‘Tuachanae’ amekiambia kipindi cha Compass Vibe cha Times FM, kuwa kabla hajatoka kimuziki alikuwa akikutana na rapa huyo wakati akifanya mazoezi THT kwa ajili ya Super Nyota.

“Msodoki mimi namkubali sana lakini pia ni mtu ambaye nilikuwa nakutana naye. Young Killer hanijui mimi lakini leo namwambia, kipindi nahustle THT alikuwa kwenye Super Nyota walikuwa wanakuja sana THT kuweka kambi hadi tukafanya tangazo fulani wote, lakini hakumbuki, yeye akaweka sauti yake mimi nikaweka yangu.,” amesema Lava Lava.

“Kwa hiyo mimi namjua kwanzia kule chini kabisa lakini yeye katika kutokumbuka kwake tukikutana tunaheshimiana,” ameongeza.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Expand
Play Cover Track Title
Track Authors