SHILOLE AMEWASAINISHA CHIPUKIZI

Posted on : June 25, 2016.   524 Views. 

Msanii wa muziki Zuwena Mohamed ‘Shilole’ ameanzisha label yake mpya ‘Shilole Entertainment’ ambapo pia amemsaini msanii chipukizi aitwae ‘Amaselly’. Muimbaji huyo ambaye anafanya vizuri na video yake ya wimbo ‘SayMyName’, amekiambia kipindi cha Clouds kuwa ameamua kuanzisha label hiyo ili kuwasaidia wasanii wenye vipaji lakini hawapati nafasi.

“Yeah nimemsani Amaselly aka Gaucho, kwa sababu ni msanii mwenye heshima, amenitafuta kwa muda mrefu, Shilole nisaidie nisaidie, kwa hiyo nikajifikiria, nikaamua kumsaidia,” alisema Shilole

Pia Shilole amesema amemsaini msanii huyo kupitia label yake mpya iitwayo Shilole Entertainment. Kwa upande wa Amasely alimshukuru Shilole kwa uwamuzi wa kumsaidia huku akihaidi mambo mazuri.

       

 
Social Media

© 2016 PRO24 DJS | All Rights Reserved!